Ingia
Ingia
Ingia
Chagua Lugha

Tafsir: Bani Israil 17:39

17:39
ذالك مما اوحى اليك ربك من الحكمة ولا تجعل مع الله الاها اخر فتلقى في جهنم ملوما مدحورا ٣٩
ذَٰلِكَ مِمَّآ أَوْحَىٰٓ إِلَيْكَ رَبُّكَ مِنَ ٱلْحِكْمَةِ ۗ وَلَا تَجْعَلْ مَعَ ٱللَّهِ إِلَـٰهًا ءَاخَرَ فَتُلْقَىٰ فِى جَهَنَّمَ مَلُومًۭا مَّدْحُورًا ٣٩
ذَٰلِكَ
مِمَّآ
أَوۡحَىٰٓ
إِلَيۡكَ
رَبُّكَ
مِنَ
ٱلۡحِكۡمَةِۗ
وَلَا
تَجۡعَلۡ
مَعَ
ٱللَّهِ
إِلَٰهًا
ءَاخَرَ
فَتُلۡقَىٰ
فِي
جَهَنَّمَ
مَلُومٗا
مَّدۡحُورًا
٣٩
Haya ni katika hikima alizo kufunulia Mola wako Mlezi. Wala usimweke pamoja na Mwenyezi Mungu mungu mwengine, usije ukatupwa katika Jahannamu ukilaumiwa na kufurushwa. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Hayo tuliyoyaeleza na kuyafafanua kati ya hizi hukumu tukufu za kuamrisha matendo mema na kukataza tabia duni, ni miongoni mwa yale tuliyokutumia wahyi nayo. Na usimfanye, ewe binadamu, pamoja na Mwenyezi Mungu yoyote kuwa ni mshirika Wake katika kumuabudu, ukaja kutiwa ndani ya moto wa Jahanamu, hali ukilaumiwa na nfsi yako na watu, na ukawa ni mwenye kufukuzwa na kuepushwa na kila kheri.